Bang Media

Friday, March 27, 2009

Usawa vs Kiburi

Usawa vs Kiburi

"After thousands of years of male dominance, we now stand at the beginning of the feminine era, when women will rise to their appropriate prominence, and the entire world will recognize the harmony between man and woman". The Rebbe.

Unakumbuka ule Mkutano wa wanawake kule Beijing au unatambua kwa nini wanawake wanaitwa "wabeijing"?

Swala la usawa baina ya wanawake na wanaume lilizua au linaendela kuzua utata kutokanana baadhi ya wanawake ku-abuse maana halisi au nia na madhumuni ya Usawa huo......na matokeo yake wanawake wamekuwa kama wanaume, wamejawa na viburi mbele za wapenzi/waume wao n.k. hii ni kutokana na kutoelewa kwa nini hasa wamama wale walikusanyana kule "Beijingi" kudai Usawa.

Ukweli ni kwamba hakuna mwanaume anataka kuwa au kuoa "mwanaume mwenzie" kwa maana kwamba unatakiwa kubaki mwanamke no matter how much you earn, no matter how educated you are, no matter how tall you are.....having said that sina maana kuwa ndio uwe kila kitu "sawa/ndio bwana/mume wangu" type.


Usawa tunaotakiwa kuutolea macho ni ule wa kujitahidi ktk elimu, ufanyaji wa kazi kwa bidii (kupata cheo kutokana na uwezo wako sio kwa jinsia yako), kuchangia maendeleo ya familia zetu na maisha yetu kwa ujumla, kuongoza au kushika nyazifa mbali-mbali ambazo awali zilidhaniwa kuwa ni za kiume tu n.k.

Usawa sio


-kuwa mlevi kwa vile wanaume wanalewa,
-kuwa na wapenzi wengi kwa vile baadhi ya wanaume wanafanya hivyo,
-kutongoza kama wanavyotongoza wanaume kwa vile tu "tuko sawa",
-kula kiasi kikubwa cha chakula kwa vile tu wanaume wanakula kuliko sisi (hushangai kwa nini wanaume wanakula sana lakini hawana pot bellies eti?) na mambo mengine mengi ambayo wanaume wanayafanya kwa sababu zao binafsi kwa vile ni wanaume au kulinda ego zao.

Ukikutana na mwanaume ambae anapenda au vutiwa na "kiburi chako" ukidhani ndio usawa ujue huyo anakuchezea na hayuko moyoni mwake

No comments:

Post a Comment