Bang Media

Sunday, March 29, 2009

Unapotengana na mpenzi

Unapotengana na mpenzi

Siku hizi watu tunaachana na wapenzi wetu sio kwa kwenda kufanya kazi mjini au kijiji cha pili bali nchi ya mbali...

Kutokana na maendeleo ya Tekinolojia na ukaribu wetu na familia tumekuwa "relaxed" pale wapenzi wetu wanapokwenda mbali nasi kwa muda mrefu ... Zamani mwanamke ukiolewa inakuwa wewe na mumeo tu sasa anapoaga kuwa nakwenda kijiji cha pili kikazi mke anakuwa ktk hali ya huzuni na kutafuta mbinu za kumshawishi mpenzi ama waende wote au asiende kabisa huko alikoagizwa.

Na hiyo huwa nafasi pakee kwa mwanamke kuonyesha kwa mpenzi wake huyo ni jinsi gani hawezi kuishi bila yeye, jinsi na kiasi gani anamhitaji mumewe na kwamba hatoweza kabisa ku-cope na upweke.

Wakati huo mwanamke alikuwa akionyesha "affection" kwa mume wake zaidi ya siku zote pale inapojuliakana lini hasa anapaswa kuondoka na siku chache kabla mpenzi hajaondoka mwanamke akipaswa kumshawishi mume/mpenzi kutokubali kusafiri au waende wote kwa kutishia kujiua (kupanda juu ya mti....sio mrefu sana na kujiachia uanguke), kulia kila siku, kususa kula nakadhalika, lakini yote hayo yakishindikana basi mwanaume anaahidi kufupisha safari yake ili awahi kurudi kuwa na mkewe/mpenzi wake.

Mume anapokuwa mbali (kasafiri) mwanamke anajitenga kwa kutokuoga mara kwa mara, kutojipamba/remba, kutokuvaa vizuri na vilevile kutotembea/toka nje bila sababu ya msingi, yote hayo ilikuwa ni mapenzi juu ya mume wake nakujaribu kuepuka kuvutia wanaume wengine na yeye mwenyewe kushawishika na ku-cheat.

Wakati huo wote mwanamke anakuwa anajifunza mbinu mbali-mbali za kumfurahisha mume/mpenzi wake au mazoezi ya jinsi ya kumpa raha mume atakaporudi, mazoezi hayo sio kukata kiuno ktk mtindo tofauti tu bali, kucheza mbele ya mume wake (strip dance sio Umagharibi ulianza miaka ya zamani ),mapishi, kuimba na wakati huohuo mwanamke hutumia muda wake kuomba Dua ili mume wake arudi salama.

Wanawake wa sasa hawajishughulishi sana kwasababu tofauti kama sio wengi wao hawajui au hawajaambiwa, vilevile ukaribu na familia na maendeleo ya Tekinolojia vinachangia kuwafanya wajisahau na kutokuwa wapweke kama zamani

No comments:

Post a Comment