Bang Media

Tuesday, March 24, 2009

Mwanamke ni "Victim"

Mwanamke ni "Victim"
-Akizaliwa ni binti wa mzee Fulani……..
-Akiolewa anakuwa mke wa Fulani…….
-Akizaa anakuwa mama Fulani…….alafu akijaaliwa nakuwa bibi fulani anamalizia na swala zima la kukabiliana na
-kukoma hedhi…..Kila hatua ya maisha yake mwanamke anakabiliana na majukumu lukuki……mwanamke huyu hajawa na nafasi ya kuwa yeye na kufurahia maisha kama yeye bali siku zote za maisha yake amekuwa akiishi kwa ajili ya watu wengine.


*Hebu tumuangalie mwanamke huyu anapofunga ndoa/ingia kwenye uhusiano…..

1)-Mimba usiku wa harusi (usiku wa kutolewa bikira).
-Mwanamke kafunga ndoa akiwa bikira na kwa bahati mbaya au nzuri wanashika mimba usiku huo au wakati wa fungate…….binti huyu hajui lolote kuhusu ngono wala utamu wake….usiku huo anafanywa kwa mara ya kwanza na mume wake anajisikia safi kuwa mkewe hakuguswa na mtu mwingine bali yeye….


Hisia za kumiliki zina mjia na bila kujali maumivu ya binti yule, haki yake ya kupata utamu au kufurahia tendo la ndoa….mume anajimalizia ndani kwa vile tu ni mke wake.

Baada ya miezi 9 mwanamke anajifungua anaanza kukuru kakara za malezi na kukabiliana na mabadiliko kutoka msichana kuwa mama…..mabadiliko haya huwa ni magumu sana as u can imagine.

Kwa vile mwanamke huyu hajui lolote kuhusu ngono na hakuwahi kufundishwa au ambiwa lolote kuhusu maswala ya mwili yeye anachukulia au kuamini kuwa kilichofanyika au kinachofanyika ni kawaida……binti anahisi kuwa labda ana kasoro kwani akikumbuka huko nyuma aliwahi kusoma, sikia, kuambiwa kuwa ukifanya mapenzi unasikia utamu au raha…..au anaona mumewe anavyofurahia….lakini masikini yeye haijui na wala hajawahi kupata utamu huo.

Mwanamke anashindwa ku-share na watu wengine kwa vile anadhani hiyo issue ni nyeti sana na ni kinyume na maadili au mila na desturi za kwao…..hivyo maisha yanaendelea na watoto wanaongezeka hali inayoongeza mabadiliko ktk mwili wake na sasa kila unapofanya mapenzi yeye ni kilio tu kutokana na maumivu (kwa vile hapati hamu ya kungonoana wala utamu wake) hali hiyo inamfanya mwanamke huyu amkwepe mumewe kwa kutafuta sababu nyingine……..


Mwanamke anaenda kulalamika kwa Daktari wake wa Magonjwa ya kike na anafanyiwa vipimo inagundulika kuwa mwanamke huyu anaelekea kwenye kukoma hedhi au kikomo cha hedhi (Menopause) kwa mwanamke huyu wa kibongo aliye ndani ya bongo kupata hamu au utamu wa kungonoana ndio inakuwa basi tena……na she is only 40yrs old.


*Ofcoz huwezi kutegemea binti wa watu bikira awe akitumia madawa ya kuzuia mimba au akujie na Condom ili azuie mimba…….wewe kama mwanaume chukua jukumu la kujizuia ili usimtie mimba binti wa watu ambe hajui chochote kuhusu unachokifanya……


Hili halitokei kwa Bikira tu bali kuna wale wanawake ambo walibakwa hivyo kisha wakaja funga ndoa, wapo walijiingiza kwenye maswala ya ngono wote wakiwa bikira hivyo hawakujifunza kitu, vilevile wapo waliokuwa kwenye uhusiano na wanaume ambao hawajali hisia za mwanamke bali tamaa zao za mwili….nakadhalika!


Wapenzi wanaume.......jaribuni kuvuta muda na mshirikishe mwanamke umpendae kwenye swala zima la kuzaa…..pangeni na muelewane mzae baada ya muda gani…..ondoa “umilikikaji” kumbuka huyo ni mkeo lakini pia ni mpenzi wako……mpe nafasi ya kuujua mwili wake kabla haujabadilika.

Chukueni jukumu la kuzuia mimba badala ya kumuachia mwanamke, kumbuka kuwa yeye mayai yake hayatoki lakini mbegu zako zinatoka na kumuingia kwenda kujenga kiumbe hivyo wewe ndio mwenye ku-control hilo na sio yeye.

Ni vema kujadiliana au kujua kama mkeo/mpenzi wako yuko tayari kukabiliana na mabadiliko yanayohusisha uzazi, kumbuka kuwa kuoa au kuwa na mpenzi sio tiketi ya kum-mimba mwenzio (cum inside).


Wanawake.......ambao mnaamini kuwa kupata mimba au kuzaa na Fulani basi ndio utapendwa zaidi au kutoachwa…… nakushauri uache huo Ujinga na Ushamba…..


Only Kubali kushika mimba ikiwa unadhani kuwa ndio kitu unachokitaka, hakikisha unajua faida, hasara, matatizo ya mimba mpaka kujifungua na baada ya kujifungua, kuwa na uhakika kuwa utakuwa tayari kukabiliana na yote hayo.


Epuka kukimbilia kuzaa/achia mimba kwa vile jamii inakukandamiza/sukuma, mtaani kwenu kila binti ana mtoto, unahofia jamii kukudhania kuwa wewe ni tasa, ili wakwe wakupende zaidi, ili mwanaume/mume asikuache au aendeleze huduma kiuchumi n.k.....


Sikutishi….bali nakwambia ukweli kuwa kushika mimba maana yake ni mabadiliko…….je unauhakika uko tayari?

Mwanamke ni victim

Mwanamke ni victim ktk kuzuia mimba.

Mwanamke siku zote ndie anaeachiwa swala la kuzuia mimba, sote tunafahamu wazi kabisa kuwa matumizi ya madawa haya ya nabadili afya ya mwanamke, yanabadili utaratibu mzima wa kupata damu ya mwezi (hedhi) kwamba kuna baadhi ya wanawake huenda mara mbili hadi tatu kwa mwezi.


Wengine hawaendi kabisa (jiulize damu hiyo inakwenda wapi wakati ni lazima itoke ikiwa yai halijarutubishwa) hali hiyo husababisha mkanganyiko wa chembechembe asilia na hivyo kusababisha SARATANI ndani ya mwili au kutopata mtoto/watoto tena….kila ukipata mimba inachoropoka (inatoka sio kwa kudhamilia) n.k.


Linapokuja swala la kumalizia ndani mwanaume hujitoa kabisa na kusukuma jukumu la kuzuia mimba kwa mwanamke. Natambua kuwa hakuna madawa ya muda mfupi yakuzuia mimba kwa wanaume lakini kuna bidhaa ambayo ikitumiwa vilivyo mimba itazuilika, sasa kwanini bidhaa hii (Condom) isitumike kwa nyote wawili badala ya “kusakizia” mwanamke jukumu hilo as if yeye ndio mhusika mkuu wa kupata ujauzito?


Ile tabia au niseme kasumba ya “situmii condom kwa vile inapunguza ukaribu wangu na mke/mpenzi wangu” haina ukweli wowote, kuwa karibu na mpenzi/mkeo wako sio lazima umalizie ndani au ugusanishe ngozi yako ya uume na ngozi yake ya uke kwa ndani!Kitendo cha wewe kufanya nae mambo mazuri na kwa ufundi yatakayowafikisha kwenye hatua hiyo tayari ni ukaribu, jinsi unavyo zungumza nae, jinsi uanvyomshika, unavyomheshimu, mthamini, unavyo onyesha mapenzi,msikiliza n.k. wakati mnafanya tendo hilo takatifu ndio mambo yatakayo kufanya uwe karibu nae a.k.a “Intimately” na sio kupiga bao ndani.


Mwanaume jaribu kuwa mbunifu na mtundu ktk anga nyingine ili kuwa “Intimate” na mkeo/mpenzi wako zaidi ya nyama 2 nyama ili kuepuka mimba na wakati huo huo kumsaidia huyu mama kulinda afya yake ili asiendelee kuwa “victim” ktk uhusiano wenu.Mwanamke ni victim ktk Ufungaji wa kizazi.

Baada yakujipatia watoto Fulani ambao mnadhani kuwa wanawatosha au ndio mnaweza kuwamudu na hivyo kufanya uamuzi wa kufunga kizai 4 good ili muweze kufanya mapenzi bila kuhofia mimba/mtoto tena, kama kawaida Mwanamke husukumwa akafunge kizazi.


Mwanamke huyu sina uhakika kama ni kasumba, ujinga, kutokujua, kuwa tegemezi au? Habishi “in good way” wala haulizi/hoji kwanini yeye ndiye anaepaswa kufanya hivyo na sio mumewe/mpenzi wake au wote....waende mguu kwa mguu kwenda kufunga kizazi?.


Mara nyingi (nimeshuhudia kwa masikio yangu) mwanaume anakuja na sababu kama “watoto wakifa kwa ajali au magonjwa na nikataka kuzaa tena nitafanyaje?”…..Ukifa (mke) na nikaoa/kutana na mwanamke mwingine na akataka kuzaa na mimi nitamwambiaje?”…..ikitokea tumeachana (peana talaka) na nikaoa tena na kutaka kuzaa na huyo mwanamke nitafanyaje?”……

Sasa huoni kuwa sababu zako za “kibinafsi” zinamhusu pia mwanamke huyo? Hayo yote yakitokea kwake yeye atafanyaje?

No comments:

Post a Comment