Bang Media

Tuesday, March 17, 2009

Mapenzi na Technologia

Mapenzi na Technologia


Vishawishi vinavyosababishwa na Teknolojia......


Sasa leo nazungumzia ni jinsi gani vitu hivi vinashawishi na hata kupelekea baadhi ya wapenzi wetu kutumia muda mwingi katika "kona" hizo kuliko ule wanatumia kuwa na sisi.

Simu za mkoni;
Ni wazi kuwa simu inarahisisha mawasiliano ya kikazi, biashara na inatufanya tuwe karibu na wapendwa wetu kila siku bila kupoteza kiasi kikubwa cha pesa kwenda kumtembelea ndugu jamaa na marafiki.

Lakini simu hizi pia zimekuwa ni kishawishi kikubwa kwetu kufanya mahusiano ya kimapenzi ya kihisia na mtu yeyote ambae anajua namba yako au wewe unajua namba yake.

Hii inaweza kutokea ikiwa mhusika mwenye jinsia tofauti na wewe anajisikia mpweke siku hiyo, amechukizwa na mpenzi wake, amesongwa na mambo mengi yanayomfanya ajisikie hana raha n.k. na hivyo akaamua kuwasiliana na wewe kwa kukutumia "text" na kila kitu kikaanzia hapo.

Vilevile mpenzi wako au wewe unaweza ukapokea "text" yenye mrindimo wa kimapenzi kutoka kwa mfanya kazi mwenzio au mfanya biashara mwenzako au hata rafiki wa mpenzi wako kimakosa, lakini kwa bahati mbaya ukavutiwa nayo (ukidhani ni yako na mhusika kakuzimia) hivyo ukaijibu vema kabisa na mpokeaji akavutiwa na ulichojibu na hapo ndio unakuwa mwanzo wa.......mambo

Hayo yote niliyoyasema na mengine unayoyajua kuhusiana na mawasiliano ya simu yakinoga huwa yanasababisha wenza wetu ku-set pin # ili usiweze kufungua simu yake(ikiwa una tabia hiyo), hata siku moja huwezi ukakuta simu yake imezagaa juu ya meza.........siku zote itabaki ndani ya bagi ambalo lina funguo, wakati wa kulala itawekwa uchagoni (chini ya mto), akiwa anaongeza nguvu simuni basi hatocheza mbali na mahali hapo n.k.
Tekinolojia na mapenzi inaendelea hapa.....Sote tunatambua kuwa mahusiano yamekuwa yakivunjika mara kwa mara, ndoa hazidumu kama ilivyokuwa miaka 40 iliyopita na kama ndoa/uhusiano huo umedumu basi ujue asilimia kubwa ni uvumilivu wa mmoja wao kwa vile kuna watoto ndani ya uhusiano huo na mara zote mvumilivu huyo huwa na uhusiano mwingine nje.

Uhusiano huo unaweza ukawa wa kimwili (mambo ya kimada, nyumba ndogo na vipoozeo), uhusiano wa kihisia tu ambao mara nyingi huitaji kuonana na mwenza wako na huu ni ule wa kimtandao a.k.a internet, uhusiano wa kimapenzi wa simu kwa kutumia sms na ule wa kuongea kwa sauti.


Mtandao a.k.a Internet.
Mtandao umekuwa sehemu kubwa ya maisha yetu hivi sasa, wengi wetu tunatumia muda mwingi kukaa mbele ya Komputa kuliko ule mda tunaotumia kukaa na wapenzi wetu.

Kwa baadhi ya wenza (couple) hujitahidi kujigawa ili mwenza wake asijisikie vibaya au kuhisi anatengwa au kutojaliwa na hivyo wapenzi hao huamua kutembelea tovuti tofauti usiku wa manene wakati wapenzi wao wamelala au ilemida ambayo wanamaliza kazi au wako kazini na kisingizio ni kuwa kuna kazi au Data wanapaswa kuzimalizia na zinahitaji uchunguzi "online".

Hapa inaweza ikawa muhusika (mwenza) akawa anatembelea chat rooms, Forums, Emails(sio zote za kikazi), kutembelea Tovuti za Porno au kama sio zile za kutafuta jamaa mliosoma pamoja, marafiki n.k.

Simu za mkononi.....sms!

Mpenzi hapa anatumia muda mwingi kutuma na kusoma sms kutoka kwa watu tofauti na baadhi huwa ni wapenzi ambapo hubandikwa majina yakiume ikiwa muhusiaka na mwanaume na kupewa majina ya kike ikiwa mhusika ni mwanaume.

Simu za mkononi-kuongea!

Mpenzi anatumia muda mwingi kuongea kwenye simu kuliko muda anaotumia kuongea au kufanya mambo mengine yanayohusiasha uhusiano wenu wa kimapenzi.

Tekinolojia hii pia inahusisha swala la kutembelea Gym, Salon......zamani hakukua na haya mambo sio, ila siku hizi utakuta bwana au bibi atumia muda mwingi kwenye kona hizo kuliko ule anaotumia na mwenza wake.

No comments:

Post a Comment