Bang Media

Friday, March 27, 2009

KUTEREZA NJE YA UHUSIANO WA KIMAPENZI

KUTEREZA NJE YA UHUSIANO WA KIMAPENZI
Umegundua kuwa mpenzi/mumeo/mkeo anatoka nje ya uhusiano wenu au yeye mwenyewe kaamua kusema kuwa hilo ndilo lililokuwa likitokea au kuendelea, -unapanic,
-inakuuma,
-unakasirika,
-unalia,
-unamfokea na kuhoji maswali lukuki kwa nini aruhusu hilo kutokea, kitu gani unakosa kwake mpaka ukatafute huko na hata kusema kuwa yule ana nini ambacho wewe huna?


Kwa kawaida hili huwa linasabaishwa na mambo mengi na kwa bahati mbaya huwa halitokei mbali au niseme na mtu ambae humjui kabisa mara nyingi huwa ni mtu wa karibu kwa maana huwa unamuona mara kwa mara, kama vile maeneo ya kazini, baa, Salon, dukani/sokoni, mfanya kazi mwenzio.


Mimi binafsi naamini kuwa hili linapotokea huwa kuna na sababu ya msingi kabisa kwa nini mmoja wenu kaamua kwenda nje nasema hivyo kwa vile naamini ktk mapenzi ya kweli na ya dhati, na imani yangu hunifanya nijue wazi kuwa hilo haliwezekani unless kuna mapungufu fulani kati yangu na mpenzi (sio upande mmoja).Lakini kwa bahati mbaya au niseme kwa kibinaadamu hili linapotokea wengi huchukulia tofauti na kujaza lawama wa yule aliyefanya kosa na hatujiulizi wenyewe kwanini ameamua kufanya hivyo towards me.


Baadhi huamua kwenda kuwaadhibu wale waliohusika na tukio zima the other woman/man kitu ambacho mimi sidhani kuwa ni busara.
Natambua hili jambo huwa linauma sana na kukufanya upoteze ile hali ya kumuamini mwenzio japo kuwa unampenda........upendo hauna maana ikiwa hakuna uaminifi, kwamba huwezi kupenda mwenzio kwa asilimia zote wakati huna imani nae tena kutokana na kosa alilofanya.


Najua kuwa kuna baadhi ya watu wanaamini kuwa wapo watu wameumbwa hivyo kwamba hata ufanye nini watatoka nje tu, ktk hali halisi hilo halipo japokuwa kuna matatizo ya kiakili (Manic Depression a.k.a Bipolar) ambayo yanaweza kumfanya mtu kufanya vitu vya ajabu ikiwa ni pamoja na kufanya ngono ovyo bila yeye kujijua yaani haamui kuwa sasa naenda kulala na fulani bali anajikuta anavutiwa na mtu nakutaka kufanya nae ngono on spot na atafanya hivyo......well hili ni tatizo la kiakili ambalo ni la kurithi na watu wachache sana wanalo.


“Cheating” imegawanyika,

-kuna wale wanaoafanya hivyo ili kuwa na mpenzi wa pili wa kudumu, kuna wale wanafanya hivyo ili kujaribu kupata mambo fulani ambayo hawayapati kwa wapenzi wao(hii huwa kwa muda mrefu) na

-kuna wale wanaofanya hivyo kwa bahati mbaya kwa vile kalewa, kashindwa kujizuia baada yakushawishiwa au alikuwa “high” kutokana na matatizo ya kiakili kama nilivyosema hapo juu.


Ni wazi kuwa hili linapotokea uamuzi wa kwanza kabisa na haraka ni kuachana na mpenzi wako, Lakini je unaweza kuendelea kuishi na mpenzi wako? Je utaweza kumuamini tena? Utaanzaje kufanya nae mapenzi? Itakuwa kama zamani au itabadilika n.k.

ATTENTION: Mpenzi anaekili kuwa ka-cheat mara nyingi huwa na mapenzi ya dhati, anajua kosa lake na pia anaumia kama unavyoumia wewe au pengine zaidi kwa kile alichokifanya na uwezekano wa yeye kurudia kosa ni mdogo sana kwa vile hatotaka kuumua au kukuumiza tena na that's love! Lakini yule anaeficha mpaka umekujakugundua affair imekuwepo kwa zaidi ya miezi kadhaa au miaka hana tofauti na muuaji na ni wazi kabisa hana mapenzi ya dhati na wewe......

Naomba niweke sawa hapa naona nimechanganya baadhi ya watu, nimesema “cheating” inaweza kuokoa uhusiano wako na sio kuwa inaokoa uhusiano wako. Hapo nina maana kuwa ikitokea mpenzi wako ame-cheat haina maana ndio mwisho wa dunia, maisha yanaweza kabisa kuendelea na penzi lenu likawa limesimama imara kama mwamba na hakuna wa kuliharibu/angusha.


Fanya uamuzi wa busara.

1.Jipe muda mbali nae na huko Jiulize je unampenda mpenzi wako? Je unadhani unaweza kumuamini tena? Unafikiri unahitaji maelezo kwanini kafanya alichofanya? Unaweza kuzungumza na marafiki zako ndugu na jamaa kuhusu tukio zima lakini waombe wasikushauru bali wakupoze nakukupa matumaini kwani ushauri wao unaweza kuharibu badala ya kujenga, wakati huu unachohitaji ni kulitafakari hilo wewe kama wewe kwani ndie pekee unaempenda, unaeishi,/uliyeishi na kumjua vema mpenzi wako.


2.Baada ya kufikiri nakutafakari ukaona mpenzi anastahili kuwa nawe basi nenda na omba maelezo ya kina kwanini kafanya alichokifanya (lazima atakuwa kisha sema mengi by now nakuomba misamaha yote) lakini msamaha kwa tafsiri yangu ni mabadiliko hivyo aliye-cheat atapaswa kuachana kabisa na mwanamke/mwanaume wa nje (unaweza ukamaliza hilo mbele ya mpenzi wako na huyo mtu wa pili), kubadili mawasiliano na kama ikiwezekana basi kazi ubadili kama sio kuhama mtaa.


Mkosaji itabidi atafute namana au njia ya kurudisha umaminifu na mapenzi kwenye ushusiano wenu. Usijilazimishe kufanya mambo ambayo unahisi yanakurudishia kumbu-kumbu ya kilichotokea hata kama hukuona lakini lazima utakuwa na hisia hizo na itakuchukua muda mrefu lakini itakwisha


Baadhi huwa wanajilazimisha kufanya mapenzi wakihofia kuwa mpenzi ataenda tena nje, ktk hali halisi jambo kubwa kama hili likitokea na ummempa nafasi ya pili mpenzi wako huwa ana-focus kwako tu na si kwingineko.....hivyo jipe muda utakao mpaka utakapo kuwa tayari.
Wewe unaesamehewa (mkosaji) usidhani kuwa mpenzi wako atasahau haraka kama alivyosamehe hivyo unatakiwa kuwa mvumilivu na kufanya kazi ya ziada ili kurudisha uaminifu na mapenzi kwa mkeo/mumeo/mpenzio.


3.Kutokana na maelezo yake ya wazi ya kwanini alifanya alichofanya lazima utahitaji kubadilika. Usibweteke kwa kudhani kuwa kwa vile yeye ni mkosaji basi ni yeye pekee ndie anapaswa kubadilika, hapana kumbuka kwenye uhusiano kunapaswa kuwa na ushirikiano ili kuufanya uhusiano huo kuwa bora (japo kuwa yeye alikuwa mbinafsi na kuchomoka nje ....), wakati yeye anajitahidi ku-re-store uaminifu na mapenzi wewe pia boresha yale ambayo ulikuwa ukizembea au kutoyafanya (inategemea na sababu iliyomfanya achoropoke).


4.Kama hali ni mbaya na mnahisi hakuna jinsi ya kuendelea na ndoa basi ni vema nyote wawili kama mtaomba msaada kwa Washauri wa ndoa kanisani na popote mnapoamini au mlipofungia ndoa, kama ni ndoa ya kiserikali basi mnaweza kujaribu Therapy ya wanandoa kwa wale ambao hawako ndoani hapa ndio huwa penye uzuri wa kutokufungana pingu za maisha kwani mtu akileta za kuleta na hakieleweki unachukua hamsini zako tu taratiiiibu (sikutumi uwe nje ya ndoa 4 life na wala sipingi ndoa ila nasema ukweli ulio wazi).

PsssT, si wanawake wengi wenye tabia hii ukilinganisha na wanaume, na ikitokea mwanamke ka-cheat mwanaume kusamehe au kuendeleza uhusiano huwa ngumu tofauti na wanawake.


Kama nilivyosema awali kuwa “cheating ziko za aina tofauti” na kuna Sababu zinazopelekea hilo kutokea. Kuna ile ya bahati mbaya ambayo inaweza kutokea leo na isitoke tena nakuna zile mbili ambazo ni zaidi ya usiku au siku moja hukua na kukomaa kabisa ambazo huwa tunaita “Affairs”.


Tofauti yake ni kuwa watu wawili wanapendana na wanajua kabisa kuwa mmoja wao au wote wako “commited” na wake/waume zao lakini wanakubaliana kuwa na uhusiano wa kingono na kimapenzi na yanaweza kabisa yakawa ya dhati.


“Affair” inaweza kushamiri, ikapendeza, ikakufunza nini maana yakupenda na kupendwa kama vile hujawahi kupenda ktk maisha yako yote na huenda ikaishia pazuri kabisa au pengine ikawa ndoa ya kwanza kwako na ya pili kwa mwenzio lakini wakati huohuo inaweza ikaharibu, kuumiza, kuchanganya, kukupotezea muda na kukatisha tamaa ya kimaisha/maendeleo, ikakupa upweke hujawahi kuupata ktk maisha yako yote kama sio kubadilisha kabisa ujinsia wako.


Sio kuwa nakubaliana na swala hili ila najaribu kuzungumzia hali halisi na kwa uwazi, unajua hii inapotokea upande mmoja huomba au kulazimisha kama sio kushawishi mpenzi wa mwenzie kuachana na yule aliyeji-commit nae ili waishi pamoja, hii inatokea mara nyingi kama mwanaume/mwanamke kaweka wazi kwa mpenzi wa nje kuwa ndoa yake sio yenye furaha kama zamani au kuna vitu havimfurahishi huko nyumbani n.k.


Huwa wanajaribu kwa hali na mali kuhakikisha unapata kile unachokitaka ili ubaki nao na usirudi ulikotoka. Kinachosikitisha na kuudhi kwenye hili ni kuwa sio wewe tu utakaeumia (mke/mume) wake bali familia nzima ikiwa ni pamoja na watoto kama mmejaaliwa kuwa nao.


Hali inapofikia hapa kung'atuka huwa ngumu kwa wewe unaeishi maisha ya aina mbili tofauti, unapaswa kuchagua moja ama kumaliza uhusiano wako wa nje kwa kuliweka wazi hilo au kuachana na mke/mume/mpenzi wako ili uwe huru kufanya ufanyalo na yeye awe huru kuishi maisha yake bila kuumizana au kutesana na wakati huohuo kuzingatia na kuthamini maisha ya baadae ya watoto na kujitahidi kuendelea kuwa wazazi japokuwa penzi halipo.


Kumbuka tu kuwa penzi halilazimishwi na kwama ukipenda au kupendwa haina maana kuwa mpenzi wako hawezi kupendwa na watu wengine, unachotakiwa kufanya ni kuboresha penzi lako kila siku na kuzingatia zaidi nini una-offer au uta-offer kwenye uhusiano wenu na sio kutegemea upande mmoja ufanya hivyo kwa vile tu umeoa/olewa au mmeoana.


Uhusiano wa mapenzi hasa ukifikia kwenye ndoa unahitaji kuufanyia kazi na kuwa mbunifu kila siku huruhusiwi kujisahau na hii sio kwa wanawake tu bali wote wake kwa waume kwani “affairs” zinafanywa na jinsi zote mbili.

Soma tena

-Yale yanayoweza kuharibu ndoa!

-Misingi ya Uhusiana wa Kimapenzi

-penzi ni nini hasa

-Kupenda kwa vitendo

Mwanaume na Mwanamke, nani anamuhitaji mwenzie?

Sababu za Kusaliti Pendo

Dalili kuwa mpenzi anatereza

No comments:

Post a Comment