Bang Media

Tuesday, March 24, 2009

Dalili za Uhusiano Unaoharibika

Dalili za Uhusiano Unaoharibika


Uchelewaji: Mmeagana kukutana na wewe umesubiri kwa takriban saa nzima, lakini anapofika ana-act kuchelewa dakika tano tu na bila aibu wala huruma haombi msamaha kwa kukugandisha vilevile hatokupa sababu ya msingi/maana (mwanamke kuchelewa kwenye “date” ni muhimu na ni sehemu ya urembo ukiachilia mbali kujiandaa kuku-impress wewe bali pia umuone wakati anaingia na kukufanya wewe ujivunie kuwa na mrembo kama yeye).

Utani:Ni kitu kizuri na husaidia kuwaweka karibu kimapenzi, lakini ikiwa mwenza wako anakutania kuhusu mambo ambayo mnayafanya mkiwa wawili tu, au kasoro zako mbele ya rafiki zake, ndugu zake na kukucheka huo hautakuwa utani bali kukudhalilisha.

Kutotilia maanani: Mfano kuna swala muhimu unataka mzungumze lakini yeye anapiga tarehe kila unapoomba muda na yeye na siku akikubali kukaa chini ili mzungumze basi majibu yake yatakuwa ndio au hapana, hatoi maelezo ya kutosha kuhusiana na issue unayomueleza hasa ikiwa inahitaji maamuzi yenu kama wenza.

Kutojali: Wakati wote wewe ni mtu wa kupiga simu kujua yuko wapi, ikiwa anaumwa au ana matatizo kifedha wewe unakuwa pale kwa ajili yake lakini kibao kikikugeukia humuoni na wala haonyeshi kujali kuwa una matatizo na kwamba anapaswa kuwa hapo kukupa moyo wa kukabiliana na yanayokukabili.

Sehemu ya mwisho ktk maisha yake: Kukatisha miadi na wewe kwa ajili ya kuonana na rafiki zake, wakati wote wote wewe ni mkosaji mbele ya wazazi wake na ndugu zake.

Kutengwa: Akitoka hatoki na wewe kwenda matembezini, kila akichelewa kurudi basi alikuwa na rafiki ambae hupaswi kumjua, hukutambulisha kwa jina lako badala ya “mpenzi wangu” ikifuatiwa na jina lako.

Kutoheshimu ndugu familia yako: Sote hatujakamilika, lakini ukikosea kidogo tu basi ukoo mzima utaunganishwa kwenye kosa hilo Mf ndio maana mama’ko yuko hivi, umerithi kutoka kwa baba yako, kwenu wote mko hivi au vile n.k.

No comments:

Post a Comment