Bang Media

Tuesday, March 24, 2009

Dalili kuwa mpenzi anatereza

Dalili kuwa mpenzi anatereza/toka nje..Unapogundua mabadiliko fulani ambayo yanahashiria kuwa mpenzi anatereza hupaswi kukasirika wala kujenga chuki na mumeo/mpenzi bali unatakiwa kuiandika upya kama sio kuibadilisha "script" kwa vile hakuna mwanaume anatoka nje bila kujua nini anakifanya, faida au hasara zake na jinsi ya kukuficha/danganya na kujitetea ikitokea atabambwa.


Kumbuka wanaume wanazungumza kama ambavyo wanawake wanafanya (hasa wakiwa hawajaoa) na swala la kutereza (cheat) linapojitokeza wote hufuata mtiririko (Script) ule ule ila wanabadili kwa kukwepa/kutofuata yale yaliyopelekea wenzao kushitukiwa kama sio kufumaniwa.


Dalili ya kwanza-

Anapopunguza "attentions" na kutumia muda wake mwingi kufanya mambo mengine ndani ya nyumba na kukufanya ujihisi/sikie "lonely in love" na unapoliweka hilo wazi anakulaumu wewe kwa kutokuwa na muda nae na wala halalamiki (najua utakavyojisikia lakini kumbuka nimesema hakuna kukasirika wala kuwa mkali) na badala yake jieleze kistaarabu kuwa huenda kufanya kwako kazi masaa mengi, kuangalia watoto au kufanya kazi nyingi ndani ya nyumba kuna kufanya uchoke sana na hivyo kutopata muda wa kuwa karibu nae lakini hiyo haina maana kuwa penzi limepungua au kuisha kwani unampenda kama mwanzo mlipokutana.


Kisha muulize ni kitu gani ambacho mlikuwa mnakifanya awali kwenye uhusiano wenu na sasa anakikosa......akimaliza kusema au kuorodhesha basi mwambie hata wewe unakosa yote hayo na ungependa mambo yawe kama yalivyokuwa awali.

Na kuanzia hapo anza kujirekebisha na kufanya mambo fulani kama mpenzi na sio mume/mwenza au mama fulani. Hapa utakuwa umegundua anatereza na wakati huohuo umezuia asiendelee kwa kumpatia kilichokuwa kikimpeleka nje (usiulize kuhusu the other woman just show him how lucky he is to have u as a wife/mwenza).


Dalili ya 2 kuwa anatereza nje...


Akishuhudia tukio lolote linalohusisha uterezaji (cheating) kutoka kwa marafiki zenu au ndugu na jamaa lenye kuhusisha swala zima la kutoka nje ya uhusiano na pea husika wanataka kuachana 4 good......atasema kwa sentensi fupi tu yenye maana kuwa "kamwe sitoweza kukufanyia hivyo" alafu kamaliza.

Najua utafurahi na kuamini kinachotoka mdomoni lakini anaweza kabisa akasema hivyo akimaanisha kuwa kamwe hutogundua anachokifanya kwa kujifunza mapungufu yaliyotokea kwenye tukio zima.....kama nilivyosema unachotakuwa kufanya hapo ni kubadili mtiririko mzima kwa kuanzisha maongezi yatakayohusisha tukio lililotokea/linalotokea bila kujenga hasira/ukali.


Kwa vile kasema kuwa yeye kamwe hatokufanyia hivyo (hatokuumiza) basi mwambie jinsi gani unampenda na namna gani utaumia au penzi lenu kusumbuka ikiwa mmoja wenu akitereza na kisha sema hutoruhusu hilo litokee kwa vile usingependa kupoteza penzi lenu.


Alafu malizia kwa kusema, lakini ikiwa mmoja wetu kashawishika na katereza nihakikishie kuwa tutalizungumza kwa uwazi na kutafuta ufumbuzi/muafaka.......hapo utakuwa umebadilisha "script" yake na wakati huohuo wewe unatakiwa kuangalia kitu gani kimepungua kama sio hakipo kwenye uhusiano wenu na hivyo anza kuki-restore taratibu ili Uhusiano usiharibike.

Pamoja na kuwa sote kazi zetu za kila siku zakutuingizia kipato ili tuendelee kuishi, kumbuka kuwa uhusiano wa kimapenzi unahitaji kufanyiwa kazi ili kuwa mzuri na wenye afya.....usitegemee penzi pekee kufanikisha hilo, unahitaji kujishughulisha kila siku ili usijisahau.(keep the fire burning).


Dalili ya 3 kuwa anachoropoka nje....


Kwa kawaida kwenye uhusiano wowote wa kimapenzi hakukosi kutofautiana na matokeo yakutofautiana ni kuzozana, sasa linapojitokeza hilo na kwa bahati mbaya hamjafikia muafaka au mmoja wenu kagoma “kukubali yaishe” au kuwa mjinga ili kutofikia pabaya basi mpenzi wako ambae “anatereza”, anaweza kuibuka na maelezo/sentensi zitakazo ashiria kuwa mnaelekea pande tofauti (hamuelewani) na kama kawaida atakurushia wewe lawama kuwa humuelewi, m-bishi au hata kuwa humheshimu.


Kwa yeye kukusingizia hayo ni wazi kuwa yatakuumiza na kukufanya labda uongeze hasira (hakuna jambo baya kama kusingiziwa jambo) lakini kama nilivyokuonya awali kuwa kukasirika hakuruhusiwi kwani tunachojaribu hapa ni kubadili “mtiririko” au “script” ili kuokoa uhusiano wenu .


Maelezo yake yako wazi (kumbuka niliwahi kusema kuwa wanaume most of the time husema kilicho kichwani), sasa hapo anakuambia kuwa uhusiano wenu hauko kama ulivyotakiwa kuwa na anaefanya au kusababisha ni wewe (hata kama ni yeye still atakusukumizia wewe) kwani sote tuna jua kwamba wanawake ndio wanaoweza kurekebisha mambo.....they are mothers, dont forget that!


Sasa ziba/zuia au ondoa hasira zako na anza kuzungumza nae taratibu kwa upendo (kama mama na mwana, yaani jisogeze...mshike panaposjikika namuangalie usoni) na kusema kuwa ungependa nyote wawili muwe kwenye mstari mmoja naje ufanye nini ili kufanikisha hilo. Kisha malizia kwa kusema kuwa utajitahidi kadiri ya uwezo wako ili kumuelewa na kurudisha heshima kwake.

Jichunguze au chunguza kuna kitu gani kimepungua ndani ya uhusiano wenu ambacho kina mfanya ahisi kuwa heshima haipo baina yenu?, kwa nini adhani kuwa hum-elewi? n.k alafu rekebisha hizo hitilafu na mambo yatakuwa poa kabisa kwani kinachomtoa nje atakuwa anakipata nyumbani.

Jambo linapojitokeza unapaswa kulizungumzia wakati huo (itakubidi ujifunze kuzuia hasira), sio unaacha siku moja au mbili zinapita alafu unarudi nyuma.....kwa mwanaume itakuwa "unapenda kulalamika kila wakati" wakati kwako itakuwa "nilihitaji muda kufikiria na kupanga maneno yangu".

Panua uwezo wako wa kiakili au niseme upeo ili uweze kufikiri haraka na kupangilia maneno cha-chap on spot, usingonjee kesho utakuta mwana sio wako.


No comments:

Post a Comment