Bang Media

Monday, March 30, 2009

Atatembea sana lakini at the end atarudi kwangu- Ukweli..

"Atatembea sana lakini at the end atarudi kwangu" Ukweli..


Mpenzi wako iwe ni mwanaume au mwanamke siku zote anakupa wakati mgumu lakini wewe unamvumilia, inafikia wakati anatoka nje ya ndoa/uhusiano wenu na kujakukuomba msamaha wewe unasamehe kwa vile tu labda unampenda, una watoto nae na usingependa watoto kumpoteza baba/mama yao au kwenda kulelewa na mtu mwingine ikiwa utamtaliki/acha mpenzio.

Umewahi kujiuliza kwa nini siku zote akikosa (wakati mwingine anakuacha kabisa) lakini baada ya muda anarudi kwako mbio akikulilia na kuomba misamaha yote kwa kuapia Miungu yote aijuayo na kukupa ahadi lukuki ili uendelee kuwa nae?

Mpenzi/mwenza mume/mke kama kweli anakupenda au nisema anakupenda kwa dhati na kukuthamini hawezi kwenda kulala nje na watu wengine na pengine kukuacha kabisa kisha ya kimshinda anarudi kwako na wewe kama juha unadhani huko ndio kupendwa, kwamba hapati "penzi" kama lako huko nje ndio mana kila wakati anarudi.

Ukweli ni kuwa mpenzi huyo anafanya hivyo kwa vile anajua wewe unampenda kwa dhati na huwezi kumuacha au kumkataa hata akuumize vipi, anahisi kuwa-secured (sio penzi) mikononi/ubavuni mwako...kumbuka usemi usemao "mpenzi akijua unampenda sana anakusumbua" hasa akiwa hana mapenzi na wewe bali yuko na wewe kwa sababu zake binafsi japokuwa alitumia au anatumia neno "nakupenda" n.k.


Sote tunatambua kuwa kuna wakati tunahitaji "mapumziko" kutoka kwenye mahusiano yetu ya kimapenzi /wenza wetu kutokana na uzito wa matatizo kikazi au kimaisha, kuna wakati mtu unahisi kwamba unataka kuwa mwenyewe bila kelele za watoto au maswali kutoka kwa mpenzi au hata "kupetiwa-petiwa" (hasa kwa wanaume pale mambo yao kiuchumi hayaendi vema).

Hili likitokea(ni tofauti ) haina maana kuwa hupendwi bali mwenzio yuko ktk wakati mgumu akifikiria jinsi ya kuilinda familia yake ikiwa ni pamoja na wewe mpenzi/mkewe na mara zote mwanaume huyo ambae anakupenda kwa dhati hatolala na mwanamke mwingine yeyote mpaka kipindi cha "mpito" kipite then atarudi kwako na kuomba radhi kwa kujiweka mbali na wewe na hata kwenda kwa kaka/rafiki yake kupumzisha akili na kupata maoni ya "kiuanaume" ambayo wewe mama huwezi kumpatia.

Hivyo wewe kama mwanamke ni vema ukaondoa hiyo kasumba au imani kuwa mumeo/mpenzi wako atatembea kote lakini lazima atarudi kwako, kwa yeye kufanya hivyo sio penzi juu yako bali penzi lako kwake ndio linamrudisha kwa vile anatambua wazi kuwa hakuna mtu atampenda kama unavyompenda wewe.

Kumbuka nia na madhumuni ya kusihi hapa Duniani kumtukuza Mungu na kufurahia maisha, hivyo ni vema kuwa kwenye uhusiano ambao nyote mnapendana na kuthaminiana, ukiona/hisi hupendwi ni vema kujitoa badala ya kuwa "unhappy na lonely in love".

unaweza kusoma tena

Sababu za Kusaliti Pendo

Dalili kuwa mpenzi anatereza

Dalili za Uhusiano Unaoharibika

Mwanaume na Mwanamke, nani anamuhitaji mwenzie?

Kupenda kwa vitendo

Misingi ya Uhusiana wa Kimapenzi

penzi ni nini hasa

No comments:

Post a Comment